Swahili

KUHUSU REDRESS

REDRESS imejitiloea kukomesha mateso na kutafuta haki kwa waathirika dunia nzima. Tunaendesha utetezi wa madai kutokana na utafiti na kwa kushirikiana na mashirika yenye mtazamo kama wetu, yaliyoundwa kwa ajili ya kupambana na ukatili wa mateso na kuwapa waathirika haki.

Kwa kupitia utafiti wa kesi, REDRESS hutoa usaidizi wa kisheria wa moja kwa moja kwa watu binafsi na jamii ambazo zimepata mateso (na uhalifu husika wa kimataifa) katika kulinda haki zao. Hii hujumuisha ushauri wa kisheria, msaada wa kuendesha madai na uwakilishi kwa waathirika katika sehemu zote duniani.

Harakati za utetezi zinalenga kuboresha hali muhimu kuwapa waathirika haki na kutaka marufuku ya kweli yapigwe juu ya mateso bila ya kikomo.

Njia za utafiti za shirika zinashawishi vizuri sera, mazoea, sheria na vigezo ili kuwezesha haki na fidia kwa waathirika.

MAADILI MUHIMU

REDRESS huweka mbele maslahi na mitazamo ya waathirika katika masuala yote ya kazi zake. Hii inamaana kwamba maamuzi na miingiliano yote ya kisheria au mingineyo, hufanyika tu baada ya kutathmini hali ya ustawi wa kijamii ya mwathirika ili kuepuka mshtuko zaidi.

Ushirikiano wa utaalam ndani na kati ya tamaduni na mabara pia ni maadili makubwa ya REDRESS. Tunashirikiana na mashirika yenye mtazamo kama wetu ili kuweza kuleta athari kubwa zaidi kadri iwezekanavyo na tunatoa msaada wa kiufundi na kusaidia mashirika ya kiraia katika jamii na pia tunasaidia mamlaka ya taifa duniani kote ili kupambana na mateso na kuwasaidia waathirika.

MSAADA KWA WAATHIRIKA

Ikiwa wewe au mwanafamilia mmewahi kuteswa na unahitaji usaidizi, inawezakana tukasaidia. REDRESS hutoa huduma zake bila ya malipo. Kutokana na uhaba wa rasilimali zetu na mambo mingine ya utendaji hatuweza kuchukua kila kesi inayokuja kwetu, lakini hata tukishindwa kuchukua kesi yako, tutajaribu kila wakati kutoa ushauri wa kitaalam ikiwezekana. Wakati mwingine pia tunaweza kukuelekeza kwenye mashirika mengine.

Ikiwa unataka tuzingatie kuchukua kesi yako:

  • Ikiwa inawezekana kwako kufanya hivyo, tafadhali jaza Fomu Yetu Mpya ya Maombi ya Kesi na tutumie kwa [email protected]. Hii itatusaidia kutathmini kama tutakuwa na uwezo wa kuchukua kesi yako. Tafadhali usiwe na hofu ikiwa huwezi kujaza baadhi ya maswali, kamilisha mengi kadri uwezavyo na tunaweza kuongea kwenye simu kuhusu maswali mengine yoyote uliyoshindwa kujibu.
  • Ikiwa huwezi kujaza Fomu Yetu Mpya ya Maombi ya Kesi, tafadhali wasiliana nasi kwa baruapepe [email protected].
  • Ni vizuri kututumia baruapepe kila wakati ikiwa unaweza, kuliko kupiga simu au kuandika barua. Hata hivyo, ikiwa huwezi kutuma baruapepe, au unahofia usalama tupigie simu kwa nambari +44 (0) 20 7793 1777 na uache maelezo mafupi, pamoja na jina lako na nambari ya mawasiliano, ili Mshauri wa Kisheria aweze kujibu simu yako.

Ili tuweze kuchukua kesi yako, tutahitaji kuamua kama kilichokutokea kinaendana na uwakili wetu na pia, kama tunaamini kwamba kuna kitu tunaweza kufanya kusaidia na tuna muda na rasilimali za kusaidia.

TAARIFA YA JUMLA YA MAWASILIANO

REDRESS UK

Unit G01, 65 Glasshill Street
London SE1 0QR, UK

Simu: +44 (0)20 7793 1777
Email: [email protected]

REDRESS Nederland

Spaarneplein 2, 2515 VK,
The Hague, The Netherlands

Simu: +31 708 919 317
Email: [email protected]